Isaya 40:27-31 Biblia Habari Njema (BHN)

27. Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo,kwa nini mnalalamika na kusema:“Mwenyezi-Mungu hatujali sisi!Mungu wetu hajali haki yetu!”

28. Je, nyinyi bado hamjui?Je, hamjapata kusikia?Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele;yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani.Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu.Maarifa yake hayachunguziki.

29. Yeye huwapa uwezo walio hafifu,wanyonge huwapa nguvu.

30. Hata vijana watafifia na kulegea;naam, wataanguka kwa uchovu.

31. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu,watapata nguvu mpya.Watapanda juu kwa mabawa kama tai;watakimbia bila kuchoka;watatembea bila kulegea.

Isaya 40