26. Inueni macho yenu juu mbinguni!Je, ni nani aliyeziumba nyota hizo?Ni yule aziongozaye kama jeshi lake,anayeijua idadi yake yote,aziitaye kila moja kwa jina lake.Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi,hakuna hata moja inayokosekana.
27. Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo,kwa nini mnalalamika na kusema:“Mwenyezi-Mungu hatujali sisi!Mungu wetu hajali haki yetu!”
28. Je, nyinyi bado hamjui?Je, hamjapata kusikia?Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele;yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani.Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu.Maarifa yake hayachunguziki.