17. Watu wenu elfu moja watamkimbia askari mmoja adui;na askari watano maadui watawakimbizeni nyote.Mwishowe, watakaosaliawatakuwa kama mlingoti wa bendera mlimani,kama alama iliyo juu ya kilima.
18. Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili,atainuka na kuwaonea huruma.Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki.Heri wote wale wanaomtumainia.
19. Enyi watu wa Siyoni, enyi watu wa Yerusalemu, hakika nyinyi hamtaomboleza tena. Kweli Mungu atawahurumia; mara tu atakaposikia kilio chenu atawaitikeni.
20. Ingawa Bwana atawalisha taabu na kuwanywesha dhiki, yeye ndiye Mwalimu wenu na hatajificha tena; nanyi mtamwona kwa macho yenu wenyewe.
21. Mkienda kulia au kushoto, mtasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Njia ni hii; ifuateni.”