Hesabu 23:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Mungu aliyewachukua kutoka Misri,huwapigania kwa nguvu kama za nyati.

23. Hakika ulozi hauwezi kuwapinga watu wa Yakobo,wala uchawi dhidi ya watu wa Israeli.Sasa kuhusu Israeli, watu watasema,‘Tazameni maajabu aliyotenda Mungu!’

24. Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike,wanasimama kama simba dume.Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake,na kunywa damu ya mawindo.”

25. Ndipo Balaki akamwambia Balaamu, “Basi, usiwalaani wala usiwabariki kabisa!”

Hesabu 23