1. Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.Mkono wa kuume wake mwenyewe,Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
2. BWANA ameufunua wokovu wake,Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
3. Amezikumbuka rehema zake,Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.Miisho yote ya dunia imeuonaWokovu wa Mungu wetu.
4. Mshangilieni BWANA, nchi yote,Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.