Zab. 97:2-7 Swahili Union Version (SUV)

2. Mawingu na giza vyamzunguka,Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.

3. Moto hutangulia mbele zake,Nao huwateketeza watesi wake pande zote.

4. Umeme wake uliuangaza ulimwengu,Nchi ikaona ikatetemeka.

5. Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA,Mbele za Bwana wa dunia yote.

6. Mbingu zimetangaza haki yake,Na watu wote wameuona utukufu wake.

7. Na waaibishwe wote waabuduo sanamu,Wajivunao kwa vitu visivyofaa;Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.

Zab. 97