Zab. 90:9-16 Swahili Union Version (SUV)

9. Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,Tumetowesha miaka yetu kama kite.

10. Siku za miaka yetu ni miaka sabini,Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;Na kiburi chake ni taabu na ubatili,Maana chapita upesi tukatokomea mara.

11. Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?

12. Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,Tujipatie moyo wa hekima.

13. Ee BWANA urudi, hata lini?Uwahurumie watumishi wako.

14. Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.

15. Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa,Kama miaka ile tuliyoona mabaya.

16. Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako,Na adhama yako kwa watoto wao.

Zab. 90