1. Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,Kizazi baada ya kizazi.
2. Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
3. Wamrudisha mtu mavumbini,usemapo, Rudini, enyi wanadamu.
4. Maana miaka elfu machoni pakoNi kama siku ya jana ikiisha kupita,Na kama kesha la usiku.
5. Wawagharikisha, huwa kama usingizi,Asubuhi huwa kama majani yameayo.
6. Asubuhi yachipuka na kumea,Jioni yakatika na kukauka.
7. Maana tumetoweshwa kwa hasira yako,Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8. Umeyaweka maovu yetu mbele zako,Siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9. Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,Tumetowesha miaka yetu kama kite.
10. Siku za miaka yetu ni miaka sabini,Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;Na kiburi chake ni taabu na ubatili,Maana chapita upesi tukatokomea mara.
11. Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?