Zab. 89:17-29 Swahili Union Version (SUV)

17. Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe,Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.

18. Maana ngao yetu ina BWANA,Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.

19. Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi,Ukasema, nimempa aliye hodari msaada;Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.

20. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,Nimempaka mafuta yangu matakatifu.

21. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake,Na mkono wangu utamtia nguvu.

22. Adui hatamwonea,Wala mwana wa uovu hatamtesa.

23. Bali nitawaponda watesi wake mbele yake,Nitawapiga wanaomchukia.

24. Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo,Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.

25. Nitaweka mkono wake juu ya bahari,Na mkono wake wa kuume juu ya mito.

26. Yeye ataniita, Wewe baba yangu,Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.

27. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza,Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.

28. Hata milele nitamwekea fadhili zangu,Na agano langu litafanyika amini kwake.

29. Wazao wake nao nitawadumisha milele,Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu.

Zab. 89