Zab. 80:1-11 Swahili Union Version (SUV)

1. Wewe uchungaye Israeli, usikie,Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi;Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.

2. Mbele ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,Uziamshe nguvu zako,Uje, utuokoe.

3. Ee Mungu, uturudishe,Uangazishe uso wako nasi tutaokoka.

4. Ee BWANA, Mungu wa majeshi, hata liniUtayaghadhibikia maombi ya watu wako?

5. Umewalisha mkate wa machozi,Umewanywesha machozi kwa kipimo kikuu.

6. Unatufanya sababu ya ugomvi kwa jirani zetu,Na adui zetu wanacheka wao kwa wao.

7. Ee Mungu wa majeshi, uturudishe,Uangazishe uso wako nasi tutaokoka.

8. Ulileta mzabibu kutoka Misri,Ukawafukuza mataifa ukaupanda.

9. Ulitengeneza nafasi mbele yake,Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi.

10. Milima ilifunikwa kwa uvuli wake,Matawi yake ni kama mierezi ya Mungu.

11. Nao uliyaeneza matawi yake hata baharini,Na vichipukizi vyake hata kunako Mto.

Zab. 80