Zab. 78:9-22 Swahili Union Version (SUV)

9. Wale Waefraimu, wenye silaha, wapiga upinde,Walirudi nyuma siku ya vita.

10. Hawakulishika agano la Mungu;Wakakataa kuenenda katika sheria yake;

11. Wakayasahau matendo yake,Na mambo yake ya ajabu aliyowaonyesha.

12. Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,Katika nchi ya Misri, konde la Soani.

13. Aliipasua bahari akawavusha;Aliyasimamisha maji mfano wa chungu.

14. Akawaongoza kwa wingu mchana,Na usiku kucha kwa nuru ya moto.

15. Akapasua miamba jangwani;Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi.

16. Akatokeza na vijito gengeni,Akatelemsha maji kama mito.

17. Lakini wakazidi kumtenda dhambi,Walipomwasi Aliye juu katika nchi ya kiu.

18. Wakamjaribu Mungu mioyoni mwaoKwa kutaka chakula kwa tamaa zao.

19. Naam, walimwamba Mungu, wakasema,Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?

20. Tazama, aliupiga mwamba;Maji yakabubujika, ikafurika mito.Pia aweza kutupa chakula?Atawaandalia watu wake nyama?

21. Hivyo BWANA aliposikia akaghadhibika;Moto ukawashwa juu ya Yakobo,Hasira nayo ikapanda juu ya Israeli.

22. Kwa kuwa hawakumwamini Mungu,Wala hawakuutumainia wokovu wake.

Zab. 78