Zab. 78:63-71 Swahili Union Version (SUV)

63. Moto ukawala vijana wao,Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

64. Makuhani wao walianguka kwa upanga,Wala wajane wao hawakuomboleza.

65. Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi,Kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo;

66. Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma,Akawatia aibu ya milele.

67. Ila akaikataa hema ya Yusufu;Wala hakuichagua kabila ya Efraimu.

68. Bali aliichagua kabila ya Yuda,Mlima Sayuni alioupenda.

69. Akajenga patakatifu pake kama vilele,Kama dunia aliyoiweka imara milele.

70. Akamchagua Daudi, mtumishi wake,Akamwondoa katika mazizi ya kondoo.

71. Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa,Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.

Zab. 78