Zab. 78:40-50 Swahili Union Version (SUV)

40. Walimwasi jangwani mara ngapi?Na kumhuzunisha nyikani!

41. Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu;Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.

42. Hawakuukumbuka mkono wake,Wala siku ile alipowakomboa na mtesi.

43. Alivyoziweka ishara zake katika Misri,Na miujiza yake katika konde la Soani.

44. Aligeuza damu mito yao,Na vijito wasipate kunywa.

45. Aliwapelekea mainzi wakawala,Na vyura wakawaharibu.

46. Akawapa tunutu mazao yao,Na nzige kazi yao.

47. Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe,Na mikuyu yao kwa mawe ya barafu.

48. Akaacha ng’ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe,Na makundi yao kwa umeme.

49. Akawapelekea ukali wa hasira yake,Ghadhabu, na uchungu, na taabu,Kundi la malaika waletao mabaya.

50. Akiifanyizia njia hasira yake;Wala hakuziepusha roho zao na mauti,Bali aliiachia tauni uhai wao;

Zab. 78