37. Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.
38. Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema,Husamehe uovu wala haangamizi.Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake,Wala haiwashi hasira yake yote.
39. Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili,Upepo upitao wala haurudi.
40. Walimwasi jangwani mara ngapi?Na kumhuzunisha nyikani!
41. Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu;Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.
42. Hawakuukumbuka mkono wake,Wala siku ile alipowakomboa na mtesi.
43. Alivyoziweka ishara zake katika Misri,Na miujiza yake katika konde la Soani.
44. Aligeuza damu mito yao,Na vijito wasipate kunywa.
45. Aliwapelekea mainzi wakawala,Na vyura wakawaharibu.
46. Akawapa tunutu mazao yao,Na nzige kazi yao.
47. Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe,Na mikuyu yao kwa mawe ya barafu.