Zab. 78:27-43 Swahili Union Version (SUV)

27. Akawanyeshea nyama kama mavumbi,Na ndege wenye mbawa,Kama mchanga wa bahari.

28. Akawaangusha kati ya matuo yao,Pande zote za maskani zao.

29. Wakala wakashiba sana;Maana aliwaletea walivyovitamani;

30. Hawakuachana na matakwa yao.Ila chakula chao kikali ki vinywani mwao

31. Hasira ya Mungu ikapanda juu yao,Akawaua waliokuwa wanono;Akawaangusha chini vijana wa Israeli.

32. Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi,Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.

33. Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi,Na miaka yao kwa hofu ya kuwasitusha.

34. Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta;Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.

35. Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao,Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao.

36. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,Wakamwambia uongo kwa ndimi zao.

37. Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake,Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.

38. Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema,Husamehe uovu wala haangamizi.Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake,Wala haiwashi hasira yake yote.

39. Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili,Upepo upitao wala haurudi.

40. Walimwasi jangwani mara ngapi?Na kumhuzunisha nyikani!

41. Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu;Wakampa mpaka Mtakatifu wa Israeli.

42. Hawakuukumbuka mkono wake,Wala siku ile alipowakomboa na mtesi.

43. Alivyoziweka ishara zake katika Misri,Na miujiza yake katika konde la Soani.

Zab. 78