Zab. 78:25-34 Swahili Union Version (SUV)

25. Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.

26. Aliuelekeza upepo wa mashariki mbinguni;Akaiongoza kusi kwa uweza wake.

27. Akawanyeshea nyama kama mavumbi,Na ndege wenye mbawa,Kama mchanga wa bahari.

28. Akawaangusha kati ya matuo yao,Pande zote za maskani zao.

29. Wakala wakashiba sana;Maana aliwaletea walivyovitamani;

30. Hawakuachana na matakwa yao.Ila chakula chao kikali ki vinywani mwao

31. Hasira ya Mungu ikapanda juu yao,Akawaua waliokuwa wanono;Akawaangusha chini vijana wa Israeli.

32. Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi,Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu.

33. Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi,Na miaka yao kwa hofu ya kuwasitusha.

34. Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta;Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii.

Zab. 78