9. Mungu amesahau fadhili zake?Amezuia kwa hasira rehema zake?
10. Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo;Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.
11. Nitayakumbuka matendo ya BWANA;Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.
12. Pia nitaitafakari kazi yako yote;Nitaziwaza habari za matendo yako.
13. Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu;Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?
14. Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.
15. Kwa mkono wako umewakomboa watu wako,Wana wa Yakobo na Yusufu.
16. Ee Mungu, yale maji yalikuona,Yale maji yalikuona, yakaogopa.Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,