Zab. 77:5-15 Swahili Union Version (SUV)

5. Nalifikiri habari za siku za kale,Miaka ya zamani zilizopita.

6. Nakumbuka wimbo wangu usiku,Nawaza moyoni mwangu,Roho yangu ikatafuta.

7. Je! Bwana atatupa milele na milele?Hatatenda fadhili tena kabisa?

8. Rehema zake zimekoma hata milele?Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?

9. Mungu amesahau fadhili zake?Amezuia kwa hasira rehema zake?

10. Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo;Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.

11. Nitayakumbuka matendo ya BWANA;Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.

12. Pia nitaitafakari kazi yako yote;Nitaziwaza habari za matendo yako.

13. Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu;Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?

14. Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.

15. Kwa mkono wako umewakomboa watu wako,Wana wa Yakobo na Yusufu.

Zab. 77