Zab. 72:11-20 Swahili Union Version (SUV)

11. Naam, wafalme wote na wamsujudie;Na mataifa yote wamtumikie.

12. Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo,Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.

13. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini,Na nafsi za wahitaji ataziokoa.

14. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu,Na damu yao ina thamani machoni pake.

15. Basi na aishi;Na wampe dhahabu ya Sheba;Na wamwombee daima;Na kumbariki mchana kutwa.

16. Na uwepo wingi wa nafakaKatika ardhi juu ya milima;Matunda yake na yawaye-waye kama Lebanoni,Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.

17. Jina lake na lidumu milele,Pindi ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;Mataifa yote na wajibariki katika yeye,Na kumwita heri.

18. Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli,Atendaye miujiza Yeye peke yake;

19. Jina lake tukufu na lihimidiwe milele;Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.

20. Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamekwisha.

Zab. 72