Zab. 69:6-14 Swahili Union Version (SUV)

6. Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe,Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi.Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe,Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

7. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu,Fedheha imenifunika uso wangu.

8. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,Na msikwao kwa wana wa mama yangu.

9. Maana wivu wa nyumba yako umenila,Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.

10. Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga,Ikawa laumu juu yangu.

11. Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu,Nikawa mithali kwao.

12. Waketio langoni hunisema,Na nyimbo za walevi hunidhihaki.

13. Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA,Wakati ukupendezao; Ee Mungu,Kwa wingi wa fadhili zako unijibu,Katika kweli ya wokovu wako.

14. Uniponye kwa kunitoa matopeni,Wala usiniache nikazama.Na niponywe nao wanaonichukia,Na katika vilindi vya maji.

Zab. 69