1. Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika,Nao wamchukiao huukimbia uso wake.
2. Kama moshi upeperushwavyo,Ndivyo uwapeperushavyo wao;Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
3. Bali wenye haki hufurahi,Na kuushangilia uso wa Mungu,Naam, hupiga kelele kwa furaha.
4. Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,Mtengenezeeni njia ya barabara,Apitaye majangwani kama mpanda farasi;Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.