Zab. 66:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,

2. Imbeni utukufu wa jina lake,Tukuzeni sifa zake.

3. Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini!Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako,Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.

4. Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,Naam, italiimbia jina lako.

5. Njoni yatazameni matendo ya Mungu;Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;

6. Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;Katika mto walivuka kwa miguu;Huko ndiko mlikomfurahia.

7. Atawala kwa uweza wake milele;Macho yake yanaangalia mataifa;Waasio wasijitukuze nafsi zao.

8. Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,Itangazeni sauti ya sifa zake;

Zab. 66