1. Ee Mungu, sifa zakulaiki katika Sayuni,Na kwako Wewe itaondolewa nadhiri.
2. Wewe usikiaye kuomba,Wote wenye mwili watakujia.
3. Ingawa maovu mengi yanamshinda,Wewe utayafunika maasi yetu.
4. Heri mtu yule umchaguaye,Na kumkaribisha akae nyuani mwako.Na tushibe wema wa nyumba yako,Patakatifu pa hekalu lako.