5. Walijifanya hodari katika jambo baya;Hushauriana juu ya kutega mitego;Husema, Ni nani atakayeiona?
6. Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,Na moyo wake, huwa siri kabisa.
7. Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,Kwa mshale mara watapigwa.
8. Ndivyo watakavyokwazwa,Ulimi wao wenyewe ukishindana nao.Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9. Na watu wote wataogopa,Wataitangaza kazi ya Mungu,Na kuyafahamu matendo yake.