Zab. 64:2-7 Swahili Union Version (SUV)

2. Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;

3. Waliounoa ulimi wao kama upanga,Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,

4. Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.

5. Walijifanya hodari katika jambo baya;Hushauriana juu ya kutega mitego;Husema, Ni nani atakayeiona?

6. Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,Na moyo wake, huwa siri kabisa.

7. Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,Kwa mshale mara watapigwa.

Zab. 64