Zab. 63:5-10 Swahili Union Version (SUV)

5. Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.

6. Ninapokukumbuka kitandani mwangu,Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.

7. Maana Wewe umekuwa msaada wangu,Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.

8. Nafsi yangu inakuandama sana;Mkono wako wa kuume unanitegemeza.

9. Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiharibu,Wataingia pande za nchi zilizo chini.

10. Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,Watakuwa riziki za mbwa-mwitu.

Zab. 63