Zab. 63:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,Nafsi yangu inakuonea kiu,Mwili wangu wakuonea shauku,Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.

2. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,Nizione nguvu zako na utukufu wako.

3. Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;Midomo yangu itakusifu.

4. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.

Zab. 63