1. Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2. Umeitetemesha nchi na kuipasua,Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.
3. Umewaonyesha watu wako mazito,Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.
4. Umewapa wakuogopao bendera,Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.
5. Ili wapenzi wako waopolewe,Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.
6. Mungu amenena kwa utakatifu wake,Nami nitashangilia.Nitaigawanya Shekemu,Nitalipima bonde la Sukothi.