1. Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu,Uniinue juu yao wanaoshindana nami.
2. Uniponye nao wafanyao maovu,Uniokoe na watu wa damu.
3. Kwa maana wanaiotea nafsi yangu;Wenye nguvu wamenikusanyikia;Ee BWANA, si kwa kosa langu,Wala si kwa hatia yangu.
4. Bila kosa langu huenda mbio, hujiweka tayari;Uamke uonane nami, na kutazama.
5. Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi,Mungu wa Israeli, uamke.Uwapatilize mataifa yote;Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja.
6. Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa,Na kuzunguka-zunguka mjini.
7. Tazama, kwa vinywa vyao huteuka,Midomoni mwao mna panga,Kwa maana ni nani asikiaye?