Zab. 56:7-12 Swahili Union Version (SUV)

7. Je! Wataokoka kwa uovu wao?Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.

8. Umehesabu kutanga-tanga kwangu;Uyatie machozi yangu katika chupa yako;(Je! Hayamo katika kitabu chako?)

9. Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;

10. Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.

11. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?

12. Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu;Nitakutolea dhabihu za kushukuru.

Zab. 56