Zab. 56:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,Mchana kutwa ananionea akileta vita.

2. Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.

3. Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

4. Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;Mwenye mwili atanitenda nini?

5. Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.

6. Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.

7. Je! Wataokoka kwa uovu wao?Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.

Zab. 56