2. Unisikilize na kunijibu,Nimetanga-tanga nikilalama na kuugua.
3. Kwa sababu ya sauti ya adui,Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu.Kwa maana wananitupia uovu,Na kwa ghadhabu wananiudhi.
4. Moyo wangu unaumia ndani yangu,Na hofu za mauti zimeniangukia.
5. Hofu na tetemeko limenijia,Na hofu kubwa imenifunikiza.
6. Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa,Ningerukia mbali na kustarehe.
7. Ningekwenda zangu mbali,Ningetua jangwani.
8. Ningefanya haraka kuzikimbiaDhoruba na tufani.
9. Ee Bwana, uwaangamize, uzichafue ndimi zao,Maana nimeona dhuluma na fitina katika mji.
10. Mchana na usiku huzunguka kutani mwake;Uovu na taabu zimo ndani yake;
11. Tamaa mbaya zimo ndani yake;Dhuluma na hila haziondoki mitaani mwake.
12. Kwa maana aliyetukana si adui;Kama ndivyo, ningevumilia.Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye;Kama ndivyo, ningejificha asinione.
13. Bali ni wewe, mtu mwenzangu,Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.
14. Tulipeana shauri tamu; na kutembeaNyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
15. Mauti na iwapate kwa ghafula,Na washuke kuzimu wangali hai,Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.