Zab. 55:12-22 Swahili Union Version (SUV)

12. Kwa maana aliyetukana si adui;Kama ndivyo, ningevumilia.Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye;Kama ndivyo, ningejificha asinione.

13. Bali ni wewe, mtu mwenzangu,Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana.

14. Tulipeana shauri tamu; na kutembeaNyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.

15. Mauti na iwapate kwa ghafula,Na washuke kuzimu wangali hai,Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.

16. Nami nitamwita Mungu,Na BWANA ataniokoa;

17. Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua,Naye ataisikia sauti yangu.

18. Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu,Maana walioshindana nami walikuwa wengi.

19. Mungu atasikia na kuwajibu;Ndiye Yeye akaaye tangu milele.Mageuzi ya mambo hayawapati hao,Kwa hiyo hawamchi Mungu.

20. Amenyosha mkono awadhuru waliopatana naye,Amelihalifu agano lake.

21. Kinywa chake ni laini kuliko siagi,Bali moyo wake ni vita.Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,Bali hayo ni panga wazi.

22. Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza,Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.

Zab. 55