Zab. 55:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee Mungu, uisikilize sala yangu,Wala usijifiche nikuombapo rehema.

2. Unisikilize na kunijibu,Nimetanga-tanga nikilalama na kuugua.

3. Kwa sababu ya sauti ya adui,Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu.Kwa maana wananitupia uovu,Na kwa ghadhabu wananiudhi.

4. Moyo wangu unaumia ndani yangu,Na hofu za mauti zimeniangukia.

5. Hofu na tetemeko limenijia,Na hofu kubwa imenifunikiza.

6. Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa,Ningerukia mbali na kustarehe.

7. Ningekwenda zangu mbali,Ningetua jangwani.

8. Ningefanya haraka kuzikimbiaDhoruba na tufani.

Zab. 55