2. Uisikie sauti ya kilio changu,Ee Mfalme wangu na Mungu wangu,Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.
3. BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu,Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.
4. Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;Mtu mwovu hatakaa kwako;
5. Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako;Unawachukia wote watendao ubatili.
6. Utawaharibu wasemao uongo;BWANA humzira mwuaji na mwenye hila
7. Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako,Nitaingia nyumbani mwako;Na kusujudu kwa kicho,Nikilielekea hekalu lako takatifu.