1. Bwana ndiye aliye mkuu,Na mwenye kusifiwa sana.Katika mji wa Mungu wetu,Katika mlima wake mtakatifu.
2. Kuinuka kwake ni mzuri sana,Ni furaha ya dunia yote.Mlima Sayuni pande za kaskazini,Mji wa Mfalme mkuu.
3. Mungu katika majumba yakeAmejijulisha kuwa ngome.
4. Maana, tazama, wafalme walikusanyika;Walipita wote pamoja.
5. Waliona, mara wakashangaa;Wakafadhaika na kukimbia.