13. Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.
14. Atapelekwa kwa mfalmeNa mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.Wanawali wenzake wanaomfuata,Watapelekwa kwako.
15. Watapelekwa kwa furaha na shangwe,Na kuingia katika nyumba ya mfalme.
16. Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako,Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.