Zab. 44:4-14 Swahili Union Version (SUV)

4. Ee Mungu, Wewe ndiwe mfalme wangu,Uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo.

5. Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu;Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao.

6. Maana sitautumainia upinde wangu,Wala upanga wangu hautaniokoa.

7. Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;Na watuchukiao umewaaibisha.

8. Tumejisifia Mungu mchana kutwa,Na jina lako tutalishukuru milele.

9. Lakini umetutupa, umetufedhehesha,Wala hutoki na majeshi yetu.

10. Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.

11. Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,Na kututawanya kati ya mataifa.

12. Wawauza watu wako bila kupata mali,Wala hukupata faida kwa thamani yao.

13. Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

14. Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa,Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.

Zab. 44