Zab. 44:10-21 Swahili Union Version (SUV)

10. Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.

11. Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,Na kututawanya kati ya mataifa.

12. Wawauza watu wako bila kupata mali,Wala hukupata faida kwa thamani yao.

13. Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

14. Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa,Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.

15. Mchana kutwa fedheha yangu i mbele yangu,Na haya ya uso wangu imenifunika,

16. Kwa sauti ya mwenye kulaumu na kukufuru,Kwa sababu ya adui na mjilipiza kisasi.

17. Haya yote yametupata, bali hatukukusahau,Wala hatukulihalifu agano lako.

18. Hatukuiacha mioyo yetu irudi nyuma,Wala hatua zetu hazikuiacha njia yako.

19. Hata utuponde katika kao la mbwa-mwitu,Na kutufunika kwa uvuli wa mauti.

20. Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu,Au kumnyoshea mungu mgeni mikono yetu;

21. Je! Mungu hatalichunguza neno hilo?Maana ndiye azijuaye siri za moyo.

Zab. 44