Zab. 41:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Heri amkumbukaye mnyonge;BWANA atamwokoa siku ya taabu.

2. BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,Naye atafanikiwa katika nchi;Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.

3. BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.Katika ugonjwa wake umemtandikia.

4. Nami nalisema, BWANA, unifadhili,Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.

5. Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,Atakufa lini, jina lake likapotea?

6. Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,Moyo wake hujikusanyia maovu,Naye atokapo nje huyanena.

Zab. 41