1. Nalimngoja BWANA kwa saburi,Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2. Akanipandisha toka shimo la uharibifu,Toka udongo wa utelezi;Akaisimamisha miguu yangu mwambani,Akaziimarisha hatua zangu.
3. Akatia wimbo mpya kinywani mwangu,Ndio sifa zake Mungu wetu.Wengi wataona na kuogopa,Nao watamtumaini BWANA
4. Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake,Wala hakuwaelekea wenye kiburi,Wala hao wanaogeukia uongo.
5. Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingiMiujiza yako na mawazo yako kwetu;Hakuna awezaye kufananishwa nawe;Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri,Ni mengi sana hayahesabiki.
6. Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,Masikio yangu umeyazibua,Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
7. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja,(Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)
8. Kuyafanya mapenzi yako,Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
9. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa.Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
10. Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.Sikuficha fadhili zako wala kweli yakoKatika kusanyiko kubwa.
11. Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako,Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.