8. Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
9. Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,Katika nuru yako tutaona nuru.
10. Uwadumishie wakujuao fadhili zako,Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
11. Mguu wa kiburi usinikaribie,Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.