1. Ee BWANA, utete nao wanaoteta nami,Upigane nao wanaopigana nami.
2. Uishike ngao na kigao,Usimame unisaidie.
3. Uutoe na mkuki uwapinge wanaonifuatia,Uiambie nafsi yangu, Mimi ni wokovu wako.
4. Waaibishwe, wafedheheshwe,Wanaoitafuta nafsi yangu.Warudishwe nyuma, wafadhaishwe,Wanaonizulia mabaya.
5. Wawe kama makapi mbele ya upepo,Malaika wa BWANA akiwaangusha chini.
6. Njia yao na iwe giza na utelezi,Malaika wa BWANA akiwafuatia.