13. Maana nimesikia masingizio ya wengi;Hofu ziko pande zote.Waliposhauriana juu yangu,Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
14. Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA,Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
15. Nyakati zangu zimo mikononi mwako;Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.
16. Umwangaze mtumishi wakoKwa nuru ya uso wako;Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
17. Ee BWANA, nisiaibishwe, maana nimekuita;Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.
18. Midomo ya uongo iwe na ububu,Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi,Kwa majivuno na dharau.
19. Jinsi zilivyo nyingi fadhili zakoUlizowawekea wakuchao;Ulizowatendea wakukimbiliaoMbele ya wanadamu!
20. Utawasitiri na fitina za watuKatika sitara ya kuwapo kwako;Utawaficha katika hemaNa mashindano ya ndimi.
21. BWANA ahimidiwe; kwa maana amenitendeaFadhili za ajabu katika mji wenye boma.
22. Nami nalisema kwa haraka yangu,Nimekatiliwa mbali na macho yako;Lakini ulisikia sauti ya dua yanguWakati nilipokulilia.
23. Mpendeni BWANA,Ninyi nyote mlio watauwa wake.BWANA huwahifadhi waaminifu,Humlipa atendaye kiburi malipo tele.