Zab. 28:4-8 Swahili Union Version (SUV)

4. Uwape sawasawa na vitendo vyao,Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao,Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao,Uwalipe stahili zao.

5. Maana hawazifahamu kazi za BWANA,Wala matendo ya mikono yake.Atawavunja wala hatawajenga;

6. Na ahimidiwe BWANA.Maana ameisikia sauti ya dua yangu;

7. BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.Moyo wangu umemtumaini,Nami nimesaidiwa;Basi, moyo wangu unashangilia,Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

8. BWANA ni nguvu za watu wake,Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.

Zab. 28