1. Ee BWANA, unihukumu mimi,Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu,Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
2. Ee BWANA, unijaribu na kunipima;Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.
3. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,Nami nimekwenda katika kweli yako.