1. Mungu wangu, Mungu wangu,Mbona umeniacha?Mbona U mbali na wokovu wangu,Na maneno ya kuugua kwangu?
2. Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibuNa wakati wa usiku lakini sipati raha.
3. Na Wewe U Mtakatifu,Uketiye juu ya sifa za Israeli.
4. Baba zetu walikutumaini Wewe,Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.