Zab. 21:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako,Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.

2. Umempa haja ya moyo wake,Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.

3. Maana umemsogezea baraka za heri,Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

4. Alikuomba uhai, ukampa,Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.

5. Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,Heshima na adhama waweka juu yake.

Zab. 21