5. Kamba za kuzimu zilinizunguka,Mitego ya mauti ikanikabili.
6. Katika shida yangu nalimwita BWANA,Na kumlalamikia Mungu wangu.Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
7. Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka,Misingi ya milima ikasuka-suka;Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
8. Kukapanda moshi kutoka puani mwake,Moto ukatoka kinywani mwake ukala,Makaa yakawashwa nao.
9. Aliziinamisha mbingu akashuka,Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.
10. Akapanda juu ya kerubi akaruka,Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo.
11. Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha,Kuwa hema yake ya kumzunguka.Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni.