Zab. 18:46-49 Swahili Union Version (SUV)

46. BWANA ndiye aliye hai;Na ahimidiwe mwamba wangu;Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu;

47. Ndiye Mungu anipatiaye kisasi;Na kuwatiisha watu chini yangu.

48. Huniponya na adui zangu;Naam, waniinua juu yao walioniinukia,Na kuniponya na mtu wa jeuri.

49. Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa,Nami nitaliimbia jina lako.

Zab. 18